UBELGIJI-SHAMBULIO-USALAMA

Mlipuko watokea katika kituo cha treni Brussels, mtuhumiwa auawa

Barabara zilizo pembezoni mwa eneo la tukio zilifungwa na magari mengi ya polisi na jeshi.
Barabara zilizo pembezoni mwa eneo la tukio zilifungwa na magari mengi ya polisi na jeshi. REUTERS/Francois Lenoir

Mlipuko unaoonekana wa kihalifu ulitokea siku ya Jumanne jioni katika kituo kikuu cha treni cha Brussels, wakati huo huo mtuhumiwa aliuawa kwa kupigwa risasi, vyombo vya habari vya Ubelgiji vimearifu. Mlipuko huo unachukuliwa kama shambulizi la kigaidi" na ofisi ya mashitaka.

Matangazo ya kibiashara

Askari wa Ubelgiji waliokua wakipiga doria katika kituo kikuu cha Brussels walifaulu kumdhibiti siku ya Jumatatu jioni mtu mmoja baada ya mlipuko mdogo, alitangaza msemaji wa polisi, akibaini kwamba hakuna hasara nyingine iliyotokea na kwamba hali ya usalama imedhibitiwa.

Kwa mujibu wa mashahidi walionukuliwa na gazeti la Het Nieuws Laatse, mtu anaetuhumiwa kutekeleza shambulio hilo alisem akwa sauti kubwa "Allaahu Akbar" kabla ya mlipuko. Kwa mujibu wa ushuhuda huu, askari walikwenda haraka eneo la tukio na kummalizia maisha.

Kufuatia mlipuko huo, hofu ilizuka katika kituo hicho, moja ya vituo vikuu mjini Brussels. Watu walioondolewa kwenye kituo hicho na shughuli ikiwa ni pamoja na usafiri vilisitishwa kwa muda. Barabara zilizo pembezoni mwa eneo la tukio zilifungwa na magari mengi ya polisi na jeshi.

Waziri Mkuu Charles Michel alitoa wito kwenyeTwitter kwa wananchi wake kufuata maelekezo ya serikali. Aliitisha haraka kikao cha baraza la mawaziri ili kutathmini hali hiyo.

Brussels ilikumbwa na mashambulizi ya kujitooa muhanga katika uwanja wa ndege na kituo cha treni za mwendo kasi mnamo mwezi Machi 2016. mji mkuu wa Ubelgiji alikuwa pia kitovu cha kusafiri kwa wanamgambo wa Kiislamu waliotekeleza mashambulizi katika mji wa Paris mnamo mwezi Novemba 2015.