UFARANSA-USALAMA

Mtu aliyejaribu kushambulia msikiti akamatwa Paris

Polisi Ufaransa imemkamata mtu aliejaribu kuvamia msikiti.
Polisi Ufaransa imemkamata mtu aliejaribu kuvamia msikiti. REUTERS/Gonzalo Fuentes

Polisi ya Ufaransa imefaulu kumkamata mtu mmoja katika jiji la Paris baada ya kujaribu kuendesha gari kwa kasi mbele ya umati wa watu nje ya msikiti mmoja nchini humo. Kwa mujibu wa maafisa wa usalama mtu huyo alikua na lengo la kuua kwa makusudi.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa maafisa wa usalama mtu huyo alikua na lengo la kuua kwa makusudi.

Polisi inasema kwamba inaendelea kumshikilia mtu huyo, na tayari uchunguzi umeanzishwa ili kujua kwamba alishirikiana na watu wengine katika kitendo hicho.

Pia polisi inasema mtu huyo hakuweza kutimiza azma yake baada ya kushindwa kuvipita vizuizi vilivyokuwepo mbele ya msikiti huo.

Vyombo vya habari vya Ufaransa vinasema mshambuliaji huyo ana asili ya Armenia.

Shambulizi hilo lilitokea katika kitongoji cha Créteil na hakuna aliyejeruhiwa.

Miaka miwili iliyopita Ufaransa ilikumbwa na mashambulizi ya kigaidi na kusababisha vifo vya watu wengi.