UJRUMANI-JAMII

Ujerumani kuhalalisha ndoa za mashoga

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akihojiwa maswali Bungeni.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akihojiwa maswali Bungeni. REUTERS/Fabrizio Bensch

Ujerumani inatazamiwa kujiunga Ijumaa hii na nchi nyingi za Magharibi kwa kuhalalisha kupitia kura za wabunge ndoa ya mashoga, baada ya Angela Merkel kuachana na upinzani wake wa maadili chini ya shinikizo la maoni ya umma.

Matangazo ya kibiashara

Angela Merkel angependelea kura hiyo ipigwe baada na bunge lijalo, baada ya uchaguzi wa wabunge mwishoni mwa mwezi Septemba, wakati wa chama chake cha kihafidhina, kilichogawanika kuhusu suala hilo, kuweza kujadili upya uwezekano wa kupitisha au la ndoa za mashoga.

Lakini baada ya kutangaza siku ya Jumatatukuwa ataacha wabunge kutoka chama chake kupiga kura kwa uhuru kuhusu suala hilo, alijikuta akilazimishwa na mshirika wake katika serikali kufanyika mara moja kwa kura ya wabunge.

Chama cha Social Democratic, ambacho kinajaribu kupata kura nyingi dhidi ya Angela Merkel katika uchaguzi wa wabunge, aliomba kupigwa kura Ijumaa hii.

Baadhi ya vigogo kutoka chama cha kihafidhina cha Angela Merkel wanapingasuala hilo lakini ni wachache katika bunge la Bundestag dhidi ya vyama vitatu vya mrengo wa kushoto, ikiwa ni pamoja chama cha SPD.