UGIRIKI-IMF-UCHUMI

IMF yakubali kutoa msaada wa Euro bilioni 1,6 kwa Ugiriki

Mkurugenzi mkuu wa IMF, Christine Lagarde.
Mkurugenzi mkuu wa IMF, Christine Lagarde. REUTERS/Hannibal Hanschke

Shirika la Fedha Duniani (IMF) siku ya Alhamisi lilikubali kutoa mkopo wa Euro bilioni 1.6 kwa nchi ya Ugiriki, na hivyo kuahidi kusaidia mpango wa tatu wa kuokoa uchumi wa nchi hiyo kwa mara ya kwanza katika miaka miwili.

Matangazo ya kibiashara

MF, hata hivyo, itatoa kiwango hicho baada ya kupokea"dhamana ya kweli na yakuaminika" kutoka wafadhili wa Ulaya wa Ugiriki juu ya muda wa kulipa deni lake, ambalo linafikia 180% ya pato la taifa (GDP).

Idhni ya IMF pia inaendana na masharti juu ya muendelezo wa mageuzi ya kiuchumi ya serikali ya Ugiriki.

Mpango huu wa kuokoa uchumi wa sasa, ambao ni wa tatu tangu mwaka 2010, unasaidiwa wakati huu na taasisi za Ulaya tu.

Uamuzi wa pili wa Bodi ya Wakurugenzi wa IMF utahitajika ili kurtekelza mpango huu wa mkopo, IMF imeongeza. Mpangilio utaisha Agosti 31, 2018, muda mfupi baada ya kumalizika kwa mpango wa msaada wa taasisi ya mseto ya Ulaya(ESM) katikati mwa mwaka 2018.

Katika mwaka 2015, IMF ilikataa kujiunga kwa mpango wa tatu wa msaada, ikibaini kwamba ni hatari kutokana na kukosekana kwa hatua za kupunguza mzigo wa madeni.

Mwezi Juni, Mkurugenzi mkuu wa IMF, Christine Lagarde, alitangaza kuwa IMF itajiunga na mpango huo wa msaada, akipendekeza kutolewa kwa fedha zilizo chini ya dola bilioni mbili.