UHISPANIA-IS-UGAIDI-USALAMA

Kundi la IS lakiri kuhusika na mashambulizi ya Barcelona

Maafisa wa polisi katika eneo la Ramblas mjini Barcelona Agosti 18, 2017, baada ya shambulio la kigaidi ambalo liliwaua watu kumi na tatu.
Maafisa wa polisi katika eneo la Ramblas mjini Barcelona Agosti 18, 2017, baada ya shambulio la kigaidi ambalo liliwaua watu kumi na tatu. REUTERS/Sergio Perez

Kundi Islamic State limekiri kuhusika na mashambulizi mjini Barcelona nchini Uhispania. Serikali ya Catalonia imesema watu 13 wamekufa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa baada ya gari la mizigo kugonga watu katika eneo la watalii la Las Ramblas, mjini Barcelona.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo polisi imesema kuwa imewakamata watu wawili. Siku ya Alhamisi jioni, maafisa wa usalama walisema kuwa walifanikiwa kuzuia shambulio la pili katika mji wa Cambril kusini magharibi mwa Barcelona. Hata hivyo washambuliaji watano waliuawa kwa mujibu wa polisi ya Catalonia.

Kundi la Islamic State (IS) kupitia shirika lake la propaganda la Amaq limetangaza kwamba ndio wamehusika na shambulizi hilo. Taarifa hii imethibitishwa na shirika la Marekani linalokagua tovuti za makundi ya kijihadi, SITE.

Vyombo vya habari vya Uhispania vimesema kuwa dereva wa gari aliliendesha na kutoroka kwa miguu baada ya kuwagonga watu kadhaa.

Maafisa wa usalama nchini Uhispania wanasema kuwa watu kadhaa wamejeruhiw watoa huduma za dharura wakiwashauri watu kukaa mbali na eneo hilo.

Ripoti kutoka eneo hilo zinasema kuwa watu walijicha ndani ya maduka yaliyo karibu, baada ya shambulio hilo.

Vikosi vya uslama na ulinzi vinaendelea kuwasaka wahusika na shambulio hilo.

Viongozi mbalimbali duniani wanaendelea kulaani shambulio hilo.

Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy amesema mashambulizi yote mawili ni ya kigaidi.

Tayari serikali ya Catalonia imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu na watu wametakiwa kukaa kimya kwa muda wa dakika moja ili kuwakumbuka waathirika wa shambulio hilo.