UHISPANIA-IS-UGAIDI-USALAMA

Dereva wa gari iliyotumiwa katika mashambulizi ya Barcelona atambuliwa

Polisi wa Catalonia katika eneo la shambulio la Las Ramblas.
Polisi wa Catalonia katika eneo la shambulio la Las Ramblas. REUTERS/Sergio Perez

Dereva wa gari ndogo nyeupe iliyogongwa watu kadhaa siku ya Alhamisi Agosti 17 katika eneo la Ramblas mjini Barcelona, na kusababisha vifo vya watu 14, ametambuliwa, polisi ya Catalonia imeandika kwenye Twitter.

Matangazo ya kibiashara

Polisi ya Uhispania inamtafuta mtuhumiwa huyo wa mwisho wa mashambulizi mawili yaliyotokea Uhispania siku ya Alhamisi. Kwa siku mbili, polisi iliweza kuangamiza kundi hili la kigaidi la watu zaidi ya kumi na mbili, wanaotuhumiwa kuhusika na madshambulizi hayo yaliyosababisha vifo vya watu 14 na wengine wengi kujeruhiwa.

Washambuliaji watano waliuawa wakati wa mashambulizi ya Cambrils, wengine wanne walikamatwa na baadhi bado wanatafutwa katika ghorofa waliokua wakiishi wanajihadi hao la Alcanar. Wachunguzi wanamsaka Abouyaaquoub Younis, raia wa Morocco mwenye umri wa miaka 22, ambaye alitoweka kabisa.

Hata hivyo polisi haijui kama mtuhumiwa huyo bado yuko Uhispania. Uchunguzi unaendeshwa katika eneo la Jonquera, kwenye mpaka na Ufaransa na Pyrenees. Polisi wa Catalonia wanafikiri kwamba Younis Abouyaaquoub aliweza kuingia nchini Ufaransa.