UJERUMANI-UCHAGUZI

Uchaguzi Ujerumani: Merkel apata ushindi kwa kura ndogo

Angela Merkel, baada ya chama cha CDU kutangazwa kuwa kimeshinda.
Angela Merkel, baada ya chama cha CDU kutangazwa kuwa kimeshinda. REUTERS/Fabrizio Bensch

Kansela wa Ujerumani amechaguliwa kuongoza nchi ya Ujerumani kwa muhula wa nne. Nderemo hazikuwa kubwa kwasababau ushindi mkuu wa uchaguzi huu ni wa AfD.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya chama chake cha CDU kupata asilimia 32.9 ya viti bungeni dhidi ya chama cha mpinzani wake Martin Schulz cha CSU kilichopata asilimia 20.8.

Kansela alitambua kwamba huenda angeshinda uchaguzi huu. Lakini sio ushindi alioutarajia yeye binfasi wala chama chake. Ni matokeo mabaya kwa chama hicho cha kihafidhina chini ya utawala wake.

Akihotubia wafuasi wa chama chake, Bi Merkel amekiri kwamba miaka minne iliyopita imekuwa migumu. Licha ya hayo chama chake kimefanikiwa kwa lengo lake kuibuka mshindi.

Baada ya ushindi huo mwishoni mwa wiki iliyopita, Kansela Merkel sasa ana kibarua cha kuongoza mazungumzo ya kuunda serikali ya pamoja na wapinzani wake.