IFARANSA-UDAIDI-USALAMA

Mtu aliyejihami kwa kisu awaua watu wawili Marseille

Polisi na askari wakielekea kwenye kituo cha treni cha Saint-Charles baada ya ya mtu aliyejihami kwa kisu kushambulia watu wawili.
Polisi na askari wakielekea kwenye kituo cha treni cha Saint-Charles baada ya ya mtu aliyejihami kwa kisu kushambulia watu wawili. Stan MARCELJA / TWITTER / AFP

Mtu aliyejihami kwa kisu aliwaua wanawake wawili katika kitio cha treni katika mji wa Saint-Charles mjini Marseille. Tukio hilo limetokea leo Jumapili Octoba 1 saa 01:45 mchana (saa za Ufaransa).

Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji ameuawa kwa kupigwa risase na askari, mkuu wa polisi ametangaza. Watu wameondolewa haraka kwenye kituo hicho cha treni. Ofisi ya mashtaka mjini Paris imetangaza kuanzisha uchunguzi kosa la mauaji yanayohusiana na ugaidi.

"Waathirika wawili wamefariki baada ya kuchomwa kisu," amesema afisa wa polisi Olivier de Mazières. Mwathirika wa kwanza aliyejichwa alifariki papo hapo, mwathirika wa pili aliuawa kwa kuchomwa kisu kifuani na tumboni, na alifariki baadaye kutokana na majeraha alioyapata. zoezi la kuwatambua waathirika hao wawili wenye umri wa miaka 20 linaendelea.

Mshambuliaji amepiga kelele akisema "Allaahu Akbar" ( "Mungu ni mkubwa") kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na uchunguzi. Chanzo hicho kinabaini kwamba kuna uwezekano kuwa shambulio hilo ni la kigaidi. Mshambuliaji huyo alikua na umri ulio kati ya miaka 25 na 30. Alitekeleza kitendo hiki peke yale. Alikuwa alijihami kwa visu viwili. Kisu kimoja kilipatikana kwenye eneo la tukio, na kingine kiliokotwa mbali kidogo na eneo la tukio. Mshambuliaji aliuawa na askari wa kikosi kinachoendesha operesheni Sentinelle ambao wanapiga doria pembezoni mwa kituo cha treni. Mshambuliaji hakuwa na kitambulisho cha uraia, kwa mujibu wagazeti la kila siku la La Provence .

Mshambuliaji huyo alikua hajulikanai katika idara inazopambana dhidi ya ugaidit. Hata hivyo alikua akijulikana na polisi kwa vitendo vya wizi mdogo.

Kulikuwa na hofu ndani ya kituo hicho cha treni ambacho kilikua kimefurika watu wengi mapem aleo mchana. Vikosi vua usalama vimewataka wakazi wa mji wa Marseille kutothubutu kufika kwenye eneo la tukio.