CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Puigdemont akataa kurejea Uhispania kwa agizo la majaji

Aliyekuwa rais wa Catalonia, Carles Puigdemont, anasita kurejea Uhispania kwa hofu ya kukamatwa.
Aliyekuwa rais wa Catalonia, Carles Puigdemont, anasita kurejea Uhispania kwa hofu ya kukamatwa. REUTERS/Ivan Alvarado

 Carles Puigdemont, rais wa Catalonia aliyetimuliwa mamlakani mwishoni mwa juma lililopita, ambaye kwa sasa yuko Brussels, hatorejea Uhispania kwa agizo la jaji mmoja wa Mahakama Kuu ya Uhispania, lakini yuko tayari kujibu maswali yake akiwa Ubelgiji, mwanasheria wake, raia wa Ubelgiji, Paul Bekaert amesema Jumatano hii.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama Kuu imeanzisha mashtaka dhidi yake kwa uasi, na uvunjaji wa uaminifu. Jaji Carmen Lamela alimtaka Carles Puigdemont kuripoti mahakamani yeye na wajumbe wengine 13 wa serikali ya Catalonia iliyofutwasiku ya Ijumaa na serikali ya Uhispania.

Kama Puigdemont hatoripoti mahakamni, hati ya kukamatwa inaweza kutolewa dhidi yake na kumzuia kushiriki katika uchaguzi wa eneo hilo ulioitishwa tarehe 21 Desemba na serikali kuu ya Uhispania, ambayo inadhibiti taasisi zote za Catalonia tangu viongozi wa Catalonia kutangaza uhuru wa wno lao.

"Hatokwenda Madrid," amesema Paul Bekaert akiliambia shirika la habari la Association Press.

"Ninapendekeza ahojiwe hapa, Ubelgiji inawezekana," Bw Bekaert ameongeza, huku akihakikisha kwamba sheria ya Uhspania inaruhusu utaratibu huo.

Carles Puigdemont, ambaye alizungumza na waandishi wa habari mjini Brussels siku ya Jumanne, alisema ataendelea kusalia nchini Ubelgiji huku akisubiri "dhamana" ya "kesi yake kutoka serikali kuu kwamba itashughulikia bila kuegemea kesi yake. Lakini aliahidi kushughulikia "changamoto ya kidemokrasia" ya uchaguzi. Aliongeza kwamba hakuwa na nia ya kutafuta hifadhi ya kisiasa au kukwepa sheria.

Viongozi watatu wa Catalonia waliomfuata Brussels walirejea siku ya Jumanne usiku Barcelona, ambapo waandamanaji waliwalaki kwa kele nyingi wakisema "gerezani".