CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Kesi kuhusu viongozi wa Catalonia yaahirishwa

Viongozi wa Catalonia wakiwasili Madrid ili kusikilizwa na mahakama ya Uhispania tarehe 2 Novemba 2017.
Viongozi wa Catalonia wakiwasili Madrid ili kusikilizwa na mahakama ya Uhispania tarehe 2 Novemba 2017. REUTERS/Susana Vera

Viongozi wa Catalonia waliotimuliwa mamlakani wamewasili Alhamisi hii NOvemba 2 mjini Madridt, ili kusikilizwa na mahakama. Wanashtumiwa kuanzisha uasi na kuchochea vurugu. Kesi hiyo imeahirishwa hadi 9 Novemba.

Matangazo ya kibiashara

Wabunge sita na wajumbe wa ofisi ya bunge, ikiwa ni pamoja na rais spika wake Carme Forcadell, waliripoti Alhamisi hii asubuhi katika Mahakama Kuu baada ya kuitishwa na Jaji ili waweze kusikilizwa. Lakini kesi hiyo imeahirishwa hadi 9 Novemba kwa ombi la wanasheria wao. Sababu ya kuahirishwa kwa kesi hiyo haijaelezewa na Mahakama Kuu, lakini wanaseria wa wanaharakati hao wa uhuru wa jimbo la Catalonia wamesema wameshanga na kuitishwa kwa wateja wao kwa muda mfupi.

Hata hivyo kiongozi wao, Carles Puigdemont, rais wa Catalonia hakuepo mahakamani kwa sababu yupo Brussels, nchini Ubelgiji, huku ripoti zikisema kuwa amekimbili nchi humo kwa hofu ya kukamatwa.

Mvutano kuhusu hali hii inayoendelea nchini Uhispania umeanza kuibua maswali mengi. Kwa upande wa serikali kuu ya Uhispania, ambayo inawachukulia viongozi wa Catalonia kwamba walikwenda kinyume cha sheria kwa kuitisha kura ya maoni iliyopigwa marufuku na kutangaza uhuru wa jimbo la Catalonia ni suala la sheria, wamesema wabunge wa Catalonia ambao wamewasili mjini Madrid, watatakiwa kujibu kwa yale wanayoshtumiwa, yaani kutoheshimu sheria za uchaguzi na Katiba, na kuruhusu kutangazwa kwa uhuru wa Catalonia.

Kwa upande wa wanaharakati wa uhuru wa jimbo la Catalonia, hata hivyo, wamebaini kwamba kesi hiyo ni ya kisiasa. Serikali ya Rajoy imekua ikitoa hoja ya sababu za kisheria kwa lengo la kuwazuia jela. Kesi yao ni ngumu kusisitiza, ndiyo sababu mawakili wa upande wa utetezi wameomba kesi hiyo kuahirishwa hadi Novemba 9.

Carles Puigdemont, kiongozi wa wanaharakati hao, anashtumiwa tuhuma nzito ikiwa ni pamoja na kuchochea vurugu na kuanzisha uasi, makosa ambayo yanaendana na adhabu ya kifungo cha miaka 30.