CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Viongozi wa Catalonia kufikishwa mbele ya majaji

Aliyekuwa rais wa Catalonia, Carles Puigdemont, anasita kurejea Uhispania kwa hofu ya kukamatwa.
Aliyekuwa rais wa Catalonia, Carles Puigdemont, anasita kurejea Uhispania kwa hofu ya kukamatwa. Reuters/路透社

Mgogoro wa Catalonia umeanza kushughulikiwa. Viongozi na wanaharakati wanaotaka uhuru wa eneo hilo wanatazamiwa kusikilizwa na majaji Alhamisi hii mjini Madrid.

Matangazo ya kibiashara

Wanashtumiwa kuanzisha uasi dhidi ya serikali kuu ya Uhispania na wanaweza kufungwa miaka 30 jela. Wakati huo kiongozi wao Carles Puigdemont akiwa mjini Brussels, nchini Ubelgiji ameiita kesi hiyo kama ya "kisiasa".

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameomba zaidi ya wajumbe wa serikali ya Catalonia walioachishwa kazi na serikali ya Madrid pamoja na Wabunge kushtakiwa kwa matumizi mabaya ya fedha za umma, kuchochea machafuko na uasi, makosa haya miwili yanaendana na adhabu ya kifungo kuanzia miaka 15 hadi 30.

Wanatuhumiwa kuhamasisha "kuanzishwa kundi la uasi" kati ya raia ili kufikia madaraka, katika mgogoro mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini Uhispania tangu mwisho wa utawala wa udikteta wa Francisco Franco katika miaka ya 1939 hadi 1975).

Licha ya kupigwa marufuku na mahakama ya Uhispania, serikali ya Catalonia ikiongozwa na Carles Puigdemont iliandaa Oktoba 1 kura ya maoni ya kuhusu uhuru wa eneo hilo.

Kura hii, ambayo hakutambuliwa na serikali kuu ya Madrid na kususiwa na vyama vinavyopambana dhidi ya uhuru, iligubikwa na vurugu za polisi, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 92, na kufuatiwa na maandamano makubwa.

Kwa mujibu wa viongozi wa Cataloni, kura ya "ndiyo" ilishindwa kwa 90.18% na kiwango cha ushiriki kilifikia 43%.

Oktoba 27, wabunge 70 kwa jumla ya 135 wa Catalonia walitangaza uhuru wa "Jamhuri ya Catalonia. Masaa machache baadaye, serikali ya Uhispania ilichukua udhibiti wa eneo hilo, huku ikifuta serikali ya jimbo hilo na bunge lake na hivyo kuitisha uchaguzi mpya mwezi Desemba 21.