UINGEREZA-SIASA-HAKI

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza ajiuzulu

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Michael Fallon.
Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Michael Fallon. REUTERS/Hannah McKay

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, Michael Fallon, anayeshutumiwa kuweka mkono wake juu ya goti la mwandishi wa habari, ametangaza kujiuzulu, msemaji wa wizara ya ulinzi amesema.

Matangazo ya kibiashara

Michael Fallon aliomba msamaha siku ya Jumatatu kwa tabia yake kwa mwandishi wa habari Julia Hartley-Brewer. Katika vyombo vya habari vya kijamii, mwandishi wa habari alitaja tukio hilo kuwa la "kujifurahisha kwa kiasi kikubwa".

Katika barua yake ya kujiuzulu aliowasilisha kwa Waziri Mkuu Theresa May, Bw. Fallon anasema kumekuwa na tuhuma nyingi dhidi za wabunge katika siku za hivi karibuni, pamoja na "baadhi kuhusu mwenendo wangu wa zamani."

"Tuhuma nyingi ni za uongo, lakini nakubali kwamba katika siku za nyuma sikifuata viwango vya juu kabisa vinavyohitajika na jeshi," Bw. Fallon aliandika. "Nimekuwa nikifikiri juu ya hali yangu na kwa hiyo ninajiuzulu kama Waziri wa Ulinzi".