CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Wakazi wa Catalonia waandamana kupinga hatua ya kuwazuia jela wanaharakati wa uhuru

Mawaziri walisikilizwa katika Mahakama ya Juu, mahakama maalumu katika kesi nyeti,  Madrid Novemba 2, 2017.
Mawaziri walisikilizwa katika Mahakama ya Juu, mahakama maalumu katika kesi nyeti, Madrid Novemba 2, 2017. REUTERS/Rafael Marchante

Maelfu ya wakaazi wa jimbo la Catalonia wameandamana mjini Barcelona kupinga kukamatwa na kuzuiwa kwa waliokuwa Mawaziri nane wa jimbo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Mawaziri hao wa zamani wanatuhumiwa kuhusika na kosa la uasi, uchochezi na matumizi mabaya ya fedha, kutokana na harakati zao za kuunga mkono kura ya maoni kutaka eneo hilo kujitenga.

Wakati huo huo, aliyekuwa kiongozi wa eneo hilo Carles Puigdemont, hakufika Mahakamani kama alivyoagizwa baada ya kusema hatafanya hivyo kwa sababu yupo jijini Brussels nchini Ubelgiji.

Viongozi wa Mashitaka wanasema wataomba hati ya kukamatwa kwa mataifa ya Umoja wa Ulaya, ili kiongozi huyo wa zamani arejeshwe nchini Uhispania na kufungiliwa mashtaka.

Wiki iliyopita, Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy alipiga marufuku uongozi wa Catalonia na kuvunja bunge la eneo hilo pamoja na kuitisha Uchagizi mpya tarehe 21 mwezi Desemba.

Serikali kuu ya Madrid imeendelea kusisitiza kuwa haiwezi kukubali kugawanyika kwa nchi ya Uhispania hata baada ya matokeo ya kura ya maoni kuonesha kuwa watu wa Jimbo la Catalonia'slonia wanataka kujitawala.