UHISPANIA

Jaji wa Uhispania atoa waranti ya kukamatwa kwa kiongozi wa Catalonia

Kiongozi aliyefutwa wa jimbo la Catalonia Carles Puigdemont
Kiongozi aliyefutwa wa jimbo la Catalonia Carles Puigdemont TV3 via REUTERS TV SPAIN OUT

Jaji nchini Uhispania jana Ijumaa ametoa waranti ya kumtaka kiongozi wa zamani wa jimbo la Catalonia Carles Puigdemont kurejea nchini humo kujibu tuhuma za uasi na matumizi mabaya ya fedha za umma pamoja na kufanya harakati za kutaka jimbo la Catalonia kujitenga na Uhispania.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo limeongeza hasira na mfadhaikoa katika usiku wa pili wa maandamano katika eneo hilo tajiri la Kaskazini Mashariki huku waandamanaji wakiimba na kupepea bendera ya Catalonia yenye mistari myekundu na njano pamoja na nyota nyeupe.

Hapo jana Umoja wa Ulaya EU ulisema hauwezi kuingilia suala la waranti ya kukamatwa kwa kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont,aliyepo nchini Ubeligiji ili arejeshwe hispania na kudai kuwa jambo hilo linazihusu mahakama za Hispania

Msemaji wa Umoja huo Annika Breidthardt amewaambia waandishi wa habari kuwa suala hilo ni la mamlaka za kimahakama ambazo uhuru wake unaheshimiwa na umoja huo kwa kiwango kikubwa.

Juhudi za Catalonia kuufanya mgogoro huo kuwa jambo la kimataifa zimegonga mwamba baada Umoja wa ulaya kuendelea kudai kuwa jambo hilo ni suala la ndani ya Hispania na wanaunga mkono umoja wa taifa hilo

Wiki moja iliyopita Puigdemont,alisimamishwa kuwa kiongozi wa jimbo hilo baada ya bunge la Catalonia kupitisha mchakato wa kutaka kujitenga na amekuwa nchini Ubeligiji tangu Jumatatu wiki hii ambapo viongozi wengine wanane wa eneo hilo wapo mahabusu wakidaiwa kujihusisha na harakati hizo.