Ubelgiji-CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Puigdemont na washauri wake waachiliwa na mahakama ya Ubelgiji

Gari lililombeba kiongozi wa Catalonia, Carles Puigdemont, akiondoka katika ofisi ya mwendesha mashitaka wa Brussels tarehe 5 Novemba 2017.
Gari lililombeba kiongozi wa Catalonia, Carles Puigdemont, akiondoka katika ofisi ya mwendesha mashitaka wa Brussels tarehe 5 Novemba 2017. Emmanuel DUNAND / AFP

Rais wa Catalonia aliyefutwa kazi, Carles Puigdemont, na washauri wake wanne ambao walijisalimisha siku ya Jumapili asubuhi Novemba 5 kwa polisi ya Ubelgiji, waliachiliwa huru jioni bila dhamana na mahakama, lakini chini ya masharti kwa kusubiri utaratibu.

Matangazo ya kibiashara

Carles Puigdemont na mawaziri wake wa zamani wa Cataloni waliachiliwa kabla ya usiku wa manane, siku ya Jumapili. Uamuzi huo ulichukuliwa na mahakama baada ya kujisalimisha kwa polisi na kukabidhiwa mahakama ya Ubelgiji.

Jaji aliyewasikiliza mchana alasiri aliamua kufuta kifungo chao kilichoanza wakati walipojisalimisha kwenye makao ya polisi siku ya Jumapili mapema asubuhi.

Carles Puigdemont na washauri wake wanne wametakiwa kuheshimu masharti matatu kwa kuepuka kukamatwa haraka. Wametakiwa kuishi ambayo ni rahisi kutambuliwa, wametakiwa kuripoti mahakamani wanapohitajika na kwa hatua zote za utaratibu, na pia wamepigwa marufuku kuondoka katika ardhi ya Ubelgiji bila idhni ya jaji anayeshughulikia kesi yao.

Hawatarudi tena Uhispania, mpaka pale ofisi ya mashitaka itabaini kwamba hatua inayofuata ya utaratibu itafanyika ndani ya wiki mbili mbele ya kitengo kiitwacho cha mahakama kitakacho amua hatma yao. Hii inaonyesha waziwazi kuwa wote watano walikataa kukubali kurejeshwa nchini Uhispania kama inavyeleza hati ya Ulaya iliyotolewa dhidi yao. Muda wa kurejeshwa nchini Uhispania ni ndani ya siku kumi tangu kutolewa kwa hati hiyo ya kukamatwa.

Carles Puigdemont na washauri wake wanashtumiwa kuchochea vurugu na uasi.