UFARANSA-MACRON-MAGEUZI

Emmanuel Macron: Nimefaulu kufanya mageuzi makubwa

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ambaye alichaguliwa Mei 7amekua akitekeleza ahadi zake za kampeni.
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ambaye alichaguliwa Mei 7amekua akitekeleza ahadi zake za kampeni. PHILIPPE WOJAZER / POOL / AFP

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kuwa amefanikiwa kuleta mageuzi makubwa nchini Ufaransa, miezi sita baada ya kuchaguliwa kwake kuwa rais wa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

"Ninafanya kile nilichosema", matamshi ya rais Emmanuel Macron, ambaye hapo jana aliongoza kikao maalum cha baraza la mawaziri pamoja na wadau engine wwa kitaifa, kunako champs Elysee, jijini Paris.

Ni miezi sita sasa tangu Macron azishike hatamu za uongozi wa taifa hilo ambapo pamoja na mambo mengine amesifia mabadiliko aliyoyataja kuwa yemeonekana hususan katika sekta ya jamii .

Miongoni mwa mabadiliko hayo Macron amesema amefurahishwa na kuboreshwa kwa maisha ya wananchi, marekebisho ya sheria za Kazi, kodi za serikali, kufutwa kwa kodi ya nyumba, kupunguzwa kwa idadi ya wanafunzi katika darasa la msingi.

Miezi sita tangu kuchaguliwa kwake, Emmanuel Macron, anasema kuwa anaendelea kuhakikisha anatekeleza ahadi alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi.

Katika tathmini yake rais Emmanuel Macron pia amesema kuwa serikali yake inafanya kila linalowezekana kuboresha masuala ya bima, kupambana na ukosefu wa ajira, lakini kubwa amesisitizia mjadala wa bajeti unaoendelea, na kuimarishwa kwa usalama wa taifa hilo.

Macron alichaguliwa kuwa rais wa Ufaransa mei 7, mwaka uliopita.