CATALONIA-UHISPANIA-MAANDAMANO-USALAMA

Maandamano makubwa kufanyika Catalonia

Muungano wa vyama vya wafanyakazi katika eneo la Catalonia  umewataka wakazi wa Catalonia kuandamana Novemba 8 (picha inayoonesha mji wa Barcelona).
Muungano wa vyama vya wafanyakazi katika eneo la Catalonia umewataka wakazi wa Catalonia kuandamana Novemba 8 (picha inayoonesha mji wa Barcelona). Otto Normalverbraucher

Muungano wa vyama vya wafanyakazi katika eneo la Catalonia umewatolea wito wakazi wa eneo hilo kumiminika mitaani Jumatano hii, huku mkutano mkubwa unaounga mkono uhuru wa eneo hilo ukitarajiwa kufanyika mjini Barcelona.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati ambapo mzozo wa kisiasa unaendelea kushuhudiwa nchini Uhispania.

Wakati huo huo Mahakama ya Brussels inatarajiwa kumsikiliza aliyekuwa rais wa Catalonia Carles Puigdemont na wajumbe wanne wa serikali yake. Wanaharakati hao wako uhamishoni nchini Ubelgiji, baada ya kufutwa kazi na serikali kuu ya Uhispania ikiungwa mkono ba bunge la nchi hiyo.

Kuna hatari Carles Puigdemont na wenzake wanne kurudishwa nchini Uhispania ili wajibu shutma dhigi yao.

Viongozi hawa wa zamani wa Catalonia wanashtumiwa uchochezi na uasi, baada ya eneo hili kujitangazia uhuru, uliopingwa na serikali kuu ya Uhispania.

Mapema wiki hii Bw. Puigdemont aliwataka viongozi wa Umoja wa Ulaya kumhakikishia kwamba wataunga mkono matokeo ya uchaguzi wa jimbo la Catalonia mwezi ujao.

Mgogoro wa kisiasa kuhusu jimbo la Catalonia unaendelea kuzua hali ya sintofahamu nchini Uhispania.