CATALONIA-UHISPANIA-MAANDAMANO-USALAMA

Shughuli nyingi zakwama kufuatia mgomo Catalonia

Catalonia yaendelea kukumbwa na maandamano makubwa.
Catalonia yaendelea kukumbwa na maandamano makubwa. REUTERS/Rafael Marchante

Mgomo ulioitishwa na muungano wa vyama vya wafanyakazi katika jimbo la Catalonia umeitikiwa na maelfu ya raia. Barabara kadhaa zilifungwa kufuatia mgomo huo, ambao pia umeathiri shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na usafiri wa treni.

Matangazo ya kibiashara

Treni ya mwendo kasi inayofanya safari za Barcelona kuelekea Lyon (Ufaransa), ilitarajiwa kufika saa 12:26 saa za Ufaransa, lakini ililazimika kurudi nyuma, kwa mujibu wa shirika la kitaifa la Reli, Renfe.

Hayo yanajiri wakati ambapo mzozo wa kisiasa unaendelea kushuhudiwa nchini Uhispania.

Wakati huo huo Mahakama ya Brussels inatarajiwa kumsikiliza aliyekuwa rais wa Catalonia Carles Puigdemont na wajumbe wanne wa serikali yake. Wanaharakati hao wako uhamishoni nchini Ubelgiji, baada ya kufutwa kazi na serikali kuu ya Uhispania ikiungwa mkono ba bunge la nchi hiyo.

Kuna hatari Carles Puigdemont na wenzake wanne kurudishwa nchini Uhispania ili wajibu shutma dhigi yao.

Viongozi hawa wa zamani wa Catalonia wanashtumiwa uchochezi na uasi, baada ya eneo hili kujitangazia uhuru, uliopingwa na serikali kuu ya Uhispania.

Mapema wiki hii Bw. Puigdemont aliwataka viongozi wa Umoja wa Ulaya kumhakikishia kwamba wataunga mkono matokeo ya uchaguzi wa jimbo la Catalonia mwezi ujao.

Mgogoro wa kisiasa kuhusu jimbo la Catalonia unaendelea kuzua hali ya sintofahamu nchini Uhispania.