CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Spika wa bunge la Catalonia kufikishwa kizimbani

Viongozi wa Cataloni waliotimuliwa mamlakani wanedelea kushikiliwa Uhispania.
Viongozi wa Cataloni waliotimuliwa mamlakani wanedelea kushikiliwa Uhispania. AFP

Siku moja baada ya mgomo katika jimbo la Catalonia, nchini Uhispania kupinga kuzuiliwa kwa viongozi wa jimbo hilo, viongozi wengine waliotimuliwa mamlakani wanatazamiwa kusikilizwa Alhamisi hii na mahakama ya Uhispania. Kuna hatari viongozi hawa kushikiliwa kwa shutma za kutangaza uhuru wa eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Spika wa bunge la Catalonia, Carme Forcadell, mwenye umri wa miaka 58, na wabunge wengine watano watakua mbele ya jaji wa Mahakama Kuu ya Madrid, Pablo Llarena, saa 9:30 asubuhi saa za Uhispania (sawa na saa 08:30 asubuhi saa za kimataifa). Jaji anatazamia kuamua ikiwa wanakabiliwa au la na uhalifu wa uasi, uchochezi na ubadhirifu wa mali ya umma katika hali ya kutangaza uhuru wa Catalonia.

Wanatuhumiwa kufuata "mkakati wa pamoja wa kutangaza uhuru," kabla ya tamko rasmi la bunge la Catalonia tarehe 27 Oktoba, tamko lililofutiliwa mbali siku ya Jumatano na Mahakama ya Katiba. Mzozo huu mbaya unaoendelea nchini Uhispania haujawahi kutokea tangu kuanza kwa mfumo wa demokrasia nchini humo miaka 40 iliopita.

Jaji huo mwenye makazi yake Catalonia kwa zaidi ya miaka 20 na mjuzi wa mambo mengi ya eneo hilo, anaweza kuamua kuwaweka kizuizini, kama wengi wa viongozi wa Catalonia walioandaa tarehe 1 Oktoba kura ya maoni kuhusu uhuru wa eneo hilo, kura ambayo ilikua ilipigwa marufuku na mahakama ya Uhispania.