CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Spika wa bunge la Catalonia kuachiliwa huru kwa dhamana

Spika wa bunge la Catalonia, Carme Forcadell, aliwasili katika Mahakama Kuu ya Madrid tarehe 9 Novemba 2017.
Spika wa bunge la Catalonia, Carme Forcadell, aliwasili katika Mahakama Kuu ya Madrid tarehe 9 Novemba 2017. AFP

Spika wa bunge la Catalonia, Carme Forcadell, amelipa Euro 150,000 kama dhamana, ambayo itamruhusu aondoke gerezani kuanzia Ijumaa hii, msemaji wa Mahakama Kuu amesema. Carme Forcadell alitakiwa kulipa dhamana hiyo kama sharti la kuachiliwa huru.

Matangazo ya kibiashara

"Dhamana ya Forcadell imepokelewa, bado kuna kusa agizo la majaji la kumuachilia huru," msemaji wa Mahakama Kuu amewaambia waandishi wa habari. Bibi Forcadell anafuatiliwa katika uchunguzi wa kuanzisha"uasi" na "uchochezi" uliozuka baada ya tangazo la uhuru lililotolewa na bunge la Catalonia Oktoba 27.Spika wa bunge la Catalonia, Carme Forcadell, mwenye umri wa miaka 58, na wabunge wengine watano walisikilizwa siku ya Alhamisi na jaji wa Mahakama Kuu ya Madrid, Pablo Llarena.

Wanatuhumiwa kufuata "mkakati wa pamoja wa kutangaza uhuru," kabla ya tamko rasmi la bunge la Catalonia tarehe 27 Oktoba, tamko lililofutiliwa mbali siku ya Jumatano na Mahakama ya Katiba. Mzozo huu mbaya unaoendelea nchini Uhispania haujawahi kutokea tangu kuanza kwa mfumo wa demokrasia nchini humo miaka 40 iliopita.

Kiongozi wa Catalonia aliyetimuliwa Carles Puigdemont na mawaziri wake wanne wako uhamishoni nchini Ubelgiji. Mapema wiki hii walisikilizwa na mahakama ya Ubelgiji, na kish wakaachiwa huru. Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel alisema katikati ya juma hili kuwa masuala ya Uhispania hayawezi kushughulikia nchini Ubelgiji.