UFARANSA-USALAMA

Visa vya kujiua vyaendelea katika vikosi vya usalama Ufaransa

Kwa jumla, polisi 61 wamejiua tangu mwanzoni mwa mwaka 2017 Ufaransa.
Kwa jumla, polisi 61 wamejiua tangu mwanzoni mwa mwaka 2017 Ufaransa. REUTERS/Gonzalo Fuentes

Visa vya kujiua vinaendelea katika vikosi vya usalama nchini Ufaransa. Antoine Boutonnet, mkuu wa zamani wa kitengo cha usalama katika viwanja vya soka, alijiua siku ya Jumapili 12 Novemba 2017.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kisa hicho Wizara ya Mambo ya Ndani mara moja ilitoa tangazo, kutaka kuanzishwa kwa mpango wa kuzuia kitendo hicho katika polisi na na idara za usalama.

Mpaka sasa idadi ya polisi na maafisa katika idara mbalimbali za usalama ambao wamejiua imefikia 61 tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

"Hakuna mtu yoyote ambaye alipatikana mpaka sasa na matatizo ya akili katika polisi," amesema Guillaume Lebeau, kutoka chama cha kuhamasisha polisi wenye hasira (MPC). Katika kesi yangu binafsi, nina saa 200 za ziada, mbali na muda wa kawaida wa kazi, na ambazo zilipwi na ni vigumu kuokoa mouda huo. Kwa sababu ili kupata muda wa ziada, unapaswa kupumzika siku kwa muda mrefu. Lakini tangu mashambulizi, tumeongezwa muda wa kufanya kazi. "

"Ni vizuri kufahamu kwamba polisi nao, ni binadamu"

Kuzidishiwa muda wa kazi na kupoteza mamlaka, kazi hii si nzuri kwa kweli Kwa mujibu wa Alexandre Langlois, kutoka chama cha polisi cha VIGI-Polisi, polisi au idara za usalama ni zinapaswa kufanyiwa mageuzi. "Tangu mwaka 1980, tumepotza wenzetu 500 ambao walifariki wakihudumu katika polisi na 1,500 ambao walijiua. Kazi ya polisi inaua mara tatu zaidi polisi kuliko majambazi na wahalifu, "Bw. Langlois amesema.

"Tunapaswa kutafakari kwamba polisi nao ni binadamu," ameongeza Alexandre Langlois. Binadamu ambao wanazidi kukabiliana na visa mbalimbali na kujiua.