AUSTRALIA-HAKI-UCHAGUZI

Australia yapiga kura kwa neema ya ndoa ya watu wa jinsia moja

Wafuasi wa ndoa za watu wa jinsia moja wakisherehekea ushindi wa kura ya "Ndiyo", Sidney, Australia Novemba 15, 2017.
Wafuasi wa ndoa za watu wa jinsia moja wakisherehekea ushindi wa kura ya "Ndiyo", Sidney, Australia Novemba 15, 2017. REUTERS/David Gray

Wananchi wa Australia wamepiga kwa wingi kura kwa neema ya ndoa ya watu wa jinsia moja, kwa karibu asilimia 62 ya kura ya "ndiyo" katika kura kwa njia ya posta iliyodumu miezi miwili.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na matokeo yaliyotolewa Jumatano hii, Novemba 15, majimbo yote na maeneo mbalimbali ya nchi hiyo walipiga kura katika mwelekeo huo. Sheria bado inahitaji kurekebishwa ili kuidhinisha kura hii.

Nchini kote Australia, maelfu ya mashabiki wa ndoa ya watu wa jinsia moja wamemiminika mitaani Jumatano hii, Novemba 15, kwa kucheza na kuimbakwa furaha ya ushindi huo.

Karibu 62% ya watu milioni 12.7 ambao walishiriki kura kwa njia ya posta, wanaounga mkono ndoa ya watu wa jinsia moja. Mamilioni ya Waustralia wamezungumzia furaha yao na walipiga kura kwa idadi kubwa kwa usawa katika ndoa," amesema Waziri Mkuu Malcolm Turnbull, ambaye anaona kura ya "Ndiyo kwa uadilifu, kujituma na upendo". Ametaka sheria ibadilishwe kabla ya Krismasi.

Kura hii imewagawa Waustralia. Waziri Mkuu wa zamani Tony Abbott amekuwa akisisitiza kwa bidii kupiga kura ya "hapana", tofauti na dada yake, Christine Forster, ambaye ni shoga.