UJERUMANI-EU-SIASA

Mgogoro wa Ujerumani waathiri Umoja wa Ulaya

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, Berlin, Novemba 20, 2017.
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, Berlin, Novemba 20, 2017. AFP

Mgogoro wa kisiasa nchini Ujerumani unamuathiri Kansela Angela Merkel, ambaye ameshindwa kuunda serikali ya mseto, lakini pia unadhoofisha Umoja wa Ulaya kwa ujumla, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

"Ujerumani imekumbwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa, na hali hii inaathiri Ulaya yote," gazeti la Le Monde limeandika.

"Wakati ambapo tunahitaji kujadili uamuzi wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya na" kujenga upya "Umoja wa Ulaya, Ujerumani inaweza kukumbwa na hali nzito kwa miezi mingi, na mradi kabambe wa Ulaya uliopendekezwa na Emmanuel Macron kunahatari ucheleweshwe,"Arnaud de La Grange amesema katika gazeti la Le Figaro.

"Malengo ya Ulaya ya Rais wa Jamhuri yako hatarini", ameongeza Luc de Barochez katika gazeti la L'Opinion.

"Kwa kushindwa kwa mazungumzo ya serikali ya mseto, (Ujerumani) kwa sasa iko kwenye mwanzo wa orodha ya nchi zinazokabiliwa na matatizo " kwa Umoja wa Ulaya, anasema Gabriel Grésillon katika gazeti la Les Echos.

"Ni pigo kubwa la ki historia" kwa taifa la kwanza lenye nguvu kiuchumi katika bara la Ulaya, taifa ambalo "kwa muda mrefu limekuwa na jukumu la kuleta utulivu katika Umoja wa Ulaya inayokabiliwa na mivutano," gazeti la kila siku la Les Echos.