CANAD-LIBYA-UTUMWA-HAKI

Canada yaomba hatua kali dhidi ya visa vya utumwa Libya

Waziri Mkuu wa Canada  Justin Trudeau.
Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau. DR

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau ameitaka jumuiya ya kimataifa kufanya jitihada dhidi ya taarifa za vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wakimbizi wa kiafrika wanaokwenda nchini Libya.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa serikali Trudeau amesema Serikali ya Canada haitakaa kimya huku ikishuhudia vitendo viovu dhidi ya binadamu.

Amesema licha ya Serikali ya Libya kuendelea kuchunguza ukiukwaji huu mkubwa wa haki za binadamu na mashirika ya kibinadamu kuanza kufanya jithada kusaidia waathirika juhudi zaidi zinatakiwa kukabiliana na vitendo hivyo viovu.

Aidha waziri huyo mkuu ammewataka wanachama wote wa Umoja wa Mataifa kuuunda na kutekeleza sheria dhidi ya usafirishaji wa binadamu hususani wanawake na watoto.

Kwa upande wake katbu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres akijibu ripoti hiyo inayohusu ukiukwaji wa haki za binadamu amesema vitendo hivyo havina nafasi katika karne ya 21.

Ripoti ya mwaka 2016 ya Marekani inasema wahamiaji kutoka ukanda wa jangwa la sahara hufika nchini libya bila nyaraka za kusafiria ambapo hulazimika kufanya kazi na wengine hujihusisha na ukahaba.