UFARANSA-VENEZUELA

Rais Macron ataka Venezuela kuwekewa vikwazo zaidi

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron REUTERS/Max Rossi

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anataka Venezuela kuwekewa vikwazo zaidi baada ya kiongozi wake Nicholas Maduro kukiuka demokrasia na haki za binadamu.

Matangazo ya kibiashara

Macron amesema inasikitisha kuona Venezuela ambayo imekuwa na demokrasia imara ya muda mrefu, kiwango hicho kikishuka sana.

“Tutakutana kama viongozi wa Ulaya, tuone ni vipi tunaweza kuiongezea vikwazo Venezuela,” alisema rais Macron.

Wito wa rais Macron umekuja baada ya Mahakama ya Juu nchini humo kuzuia chama kikuu cha upinzani Democratic Union Roundtable (MUD) kushiriki katika Uchaguzi wa urais utakaofanyika mwezi Aprili mwaka huu.

Hatua hii inamwacha rais Nicholas Maduro kuwa mgombea pekee katika uchaguzo huo.

Mahakama wiki hii, ilisitisha zoezi la kupitia upya vyama vya siasa nchini humo, zoezi ambalo linastahili kuchukua muda wa miezi sita kwa mujibu wa sheria.

Mahakama hiyo imesema kuwa, chama hicho hakiwezi kusajiliwa kwa sababu ni muungano wa vyama vya upinzani nchini humo.

Rais Maduro, ameunga mkono Uchaguzi huo ambao amesema utairejeshea heshima nchi yake.