UJERUMANI-SIASA

Chama cha Kansela wa Ujerumani chakabiliwa na mgawanyiko

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel (katikati), Horst Seehofer (CSU) na Martin Schulz (SPD), Januari 12 Berlin.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel (katikati), Horst Seehofer (CSU) na Martin Schulz (SPD), Januari 12 Berlin. REUTERS/Hannibal Hanschke

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na vigogo wengine katika chama chake cha CDU wanatarajia kupitisha leo Jumatatu rasimu ya serikali katika hali ya kuiondoa nchi hiyo katika hali ya sintofahamu baada ya kushindwa kuunda serikali ya umoja.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo chama cha CDU kinakabiliwa na hatari ya kugawanyika.

Wajumbe elfu moja wa chama hicho wanatarajia kukutana leo Jumatatu mchana katika mkutano mkuu wa chama mjini Berlin.

Lengo kuu ni kupitisha mkataba wa muungano uliojadiliwa mapema mwezi huu kati ya chama cha CDU, mshirika wake CSU na chama cha SPD, baada ya zaidi ya miezi minne ya ya mvutano katika mazingira ya kisiasa uliozuka baada ya uchaguzi wa wabunge mnamo mwezi Septemba.

Katika hali ya kushawishi chama cha SPD ambacho kilisita mara kadhaa kujiunga na chama cha CDU, Angela Merkel alikubali kukipa chama hicho wizara ya fedha, inayoonekana kama uti wa uchumi nchini Ujerumani na Ulaya.