UINGEREZA-USALAMA

Mlipuko waua watu wanne Leicester, Uingereza

Polisi ya Uingereza inasema kuwa  operesheni ya uokoaji inaendelea kuwapata waathirika wengine huko Leicester.
Polisi ya Uingereza inasema kuwa operesheni ya uokoaji inaendelea kuwapata waathirika wengine huko Leicester. AFP

Watu wanne walipoteza maisha katika mlipuko uliotokea katika jengo moja jana Jumapili usiku huko Leicester, nchini Uingereza. Mlipuko huo hauna uhusiano wowote na kitendo cha kigaidi, polisi wa Uingereza imesema leo Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

"Watu wanne walipoteza maisha katika mlipuko uliyotokea katika jengo moja hukoLeicester jana usiku," polisi imesema katika taarifa yake.

Aidha, watu wanne bado wanalazwa hospitali, ikiwa ni pamoja na moja ambaye amepata majeraha makubwa, imesema polisi ya mji huo ulio katikati mwa Uingereza.

Jengo lililokumbwa na mlipuko huo "lilikuwa na nafasi ya kibiashara kwenye ghorofa ya chini na makazi ya watu kwenye ghorofa ya juu. Tunafikiri kunaweza kuwa na watu ambao bado wamekwama huko na operesheni ya uokoaji inaendelea kuwapata waathirika wengine, "Shane O'Neill afisa katika mji huo, amenukuliwa katikataarifa hiyo.

"Mara tu eneo hilo litakua salama, uchunguzi utafanyika na idara ya huduma za uokoaji na majanga ya moto kuchunguza mazingira ya tukio hilo, ambayo kwa hadi sasa hakuna uhusiano wowote na kitendo cha ugaidi," ameongeza.