EU-MAREKANI

Marekani, EU zatangaza kuwafurusha wanadiplomasia wa Urusi

Rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa Marekani Donald Trump. REUTERS/Leah Millis

Nchi ya Marekani pamoja na mataifa mengine manne kwenye umoja wa Ulaya wametangaza kuwafurusha kwenye nchi zao wanadiplomasia wa Urusi baada ya tukio la sumu la jijini London majuma kadhaa yaliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Donald Trump kwa upande wake ameagiza kufukuzwa nchini humo kwa maafisa 60 wanaodaiwa kuwa ni majasusi wa Urusi katika kile kinachoonekana ni kujibu mapigo kutokana na tukio la kupewa sumu kwa jasusi wake wa zamabi mjini Salisbury.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Sarah Sanders amesema hatua hiyo imetokana na juhudi za kidunia dhidi ya Urusi hatua zilizochukuliwa baada ya Urusi kudaiwa kutumia simu yenye kemikali kwenye ardhi ya Uingereza.

Marekani inasema maofisa 48 ambao hawajulikani wako Marekani na wengine 12 kwenye umoja wa Mataifa na sasa wanazo siku 4 kuondoka.

Rais Trump pia ameagiza kufungwa kwa ofisi za ubalozi wa Urusi mjini Seattle, ofisi ambazo Marekani inasema zilikuwa zinatumiwa na Urusi kufanya ujasusi.

Katika hatua nyingine mataifa 14 ya kwenye umoja wa Ulaya yanawafurusha wanadiplomasia wa Urusi katika kile kinachoonekana ni kuungana na nchi ya Uingereza dhidi ya Urusi inayotuhumiwa kutumia sumu dhidi ya jasusi wake wa zamani.

“Katika kutekeleza makubaliano ya wakuu wa nchi ya juma lililopita kuhusu kitendo cha Urusi, hii leo mataifa 14 yameridhia kuwafurusha wanadiplomasia hao,” amesema rais wa umoja wa Ulaya Donald Tusk.

Uamuzi huu wa nchi za Ulaya umekuja baada ya waziri mkuu Theres May kuwahutubia wenzake kwenye umoja wa Ulaya jiji Brussels kuwataka wamuunge mkono kutokana na tathmini iliyofanywa na nchi yake kuhusu Urusi.

Nchi wanachama 28 zilitoa taarifa zikisema wamekubaliana kuwa kuna uwezekano mkubwa Urusi inahusika na tukio la kumshambulia kwa sumu Sergei Skripa na mtoto wake Yulia mwezi Machi mwaka huu na kumwitisha balozi wake mjini Moscow.