UFARANSA-MAREKANI-USHIRIKIANO

Emmanuel Macron kuzuru Marekani

Rais wa Ufaransa na mkewe wanawasili Jumatatu wiki hii, Aprili 23 mjini Washington, nchini Marekani, kwa ziara ya kwanza ya kiserikali iliyoandaliwa na Rais Trump tangu kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atakutana na mwenyeji wake rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atakutana na mwenyeji wake rais wa Marekani Donald Trump. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizi mbili zinaendelea na uhusiano wao mzuri. Lakini wawili hawa wanatarajia kuzungumzia masuala mengi ikiwa ni pamoja na suala la mpango wa nyuklia wa Iran na masuala ya biashara.

Uhusiano mzuri kati ya marais wa Ufaransa na Marekani umekua mara kwa mara ukijadiliwa mjini Paris na Washington, ambapo wengi wanabaini kuepo kwa masuala nyeti yanayofanana kwa nchi hizo mbili: wote wawili wamejikita katika sekta binafsi, matokeo yao ya uchaguzi yalipiga rikodi, na wanaonesha nia yao ya kubadili njia ya kufanya siasa.

Lakini marais hawa wametofautiana katika masuala kadhaa. Hasa kuhusu mapambano katika mabadiliko ya tabia nchi, na kujiondoa kwa Washington kwenye mkataba wa Paris, au kwenye biashara, na kuanza kutekelezwa mnamo Mei 1 kodi mpya za Marekani kwa chuma na aluminium kwa Ulaya.

Miongoni mwa masuala yenye uzito mkubwa upande wa Marekani ambayo Emmanuel Macron anatarajia kuyapa kipaumbele, kuna hasa makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran. Rais Trump alitoa muda hadi Mei 12 kwa  nchi waliosaini mkataba huo kwa kile lichokiita "mapungufu ya kutisha" kwenye mkataba huo, la sivyo atakataa kuongeza muda wa vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.