UBELGIJI-UGAIDI

Ugaidi: Salah Abdeslam ahukumiwa kufungwa miaka 20 jela

Wakati mahakma ya Ubelgiji ikitoa hukumu ya kufungwa miaka 20 jela dhidi ya Salah Abdeslam, Aprili 23, 2018.
Wakati mahakma ya Ubelgiji ikitoa hukumu ya kufungwa miaka 20 jela dhidi ya Salah Abdeslam, Aprili 23, 2018. Frederic Sierakowski/Pool via REUTERS

Mahakama ya Ubelgiji imemhukumu Salah Abdeslam kifungo cha miaka 20 baada ya kupatikana na hatia inayohusiana na mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea Paris mnamo mwa 2015.

Matangazo ya kibiashara

Salah Abdeslam ni mmoja wa magaidi waliotekelesha mashambulizi ya kigaidi tarehe 13 Novemba 2015 nchini Ufaransa. Amehukumiwa mjini Brussels kwa kosa la kujaribu kuua maafisa wa polisi.

Wakati wa urushianaji risasi mwaka 2016 wilayani Forest, muda mfupi kabla ya kukamatwa, aliwajeruhi maafisa kadhaa wa polisi, ikiwa ni pamoja na mmoja ambaye alikua alijeruhiwa vibaya.

Inadaiwa kuwa tukio hilo lilikuja kabla ya maandalizi ya mashambulizi ya Brussels wiki moja baadaye, tarehe 22 Machi.

Awali viongozi wa Mashtaka walitaka Abdeslam na mshtakiwa mwezake Sofiane Ayari kufungwa jela miaka 20 kwa makosa ya kigaidi na kumiliki silaha zilizopigwa marufuku. wengi kujeruhiwa.