Pata taarifa kuu
ITALIA-SIASA

Baraza jipya la mawaziri kuapishwa Italia

Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte.
Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte. REUTERS/Alessandro Bianchi

Hatimae wanasiasa nchini Italia wamekubaliana kuhusu kuundwa kwa serikali ya Muungano baada ya miezi takriban miezi mitatu ya mvutano katika taifa hilo la nne lenye uchumi mkubwa katika Umoja wa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Giuseppe Conte amewasilisha orodha ya baraza la mawaziri kwa Rais Sergio Mattarella ikiwa ni mara ya pili juma hili ambae ameikubali orodha hiyo na sasa serikali hiyo mpya itakula kiapo baadae Ijumaa hii Juni 1.

Mawaziri ni kutoka pande zote mbili zilizokuwa zikivutana, ikiwa ni upande wa vuguvugu linalojiita Nyota 5 (M5S) na ule lile liitwalo ligi ya kulia

Awali rais Mattarella alikataa orodha iliokuwa imewasilishwa na Waziri Mkuu Conte kutokana na jina la waziri wa uchumi ambae rais alililkataa, lakini baada ya kubadilishwa hatimae rais amekubali baraza hilo baada ya kupewa uhakika wa Italia kubaki katika ukanda wa Euro.

Serikali hiyo mpya itaongozwa na Giuseppe Conte, Mhadhiri wa chuo kikuu wa maswala ya sheria na wakili mwenye umri wa miaka 53 na alikuwa hajulikani na pande zote mbili wakati alipoteuliwa siku 15 zilizopita.

Hadi Alhamisi wiki hii alikuwa chuoni akitoa visomo katika chuo kikuu cha Florence na ndie atawakilisha Italia juma lijalo katika mkutano wa nchi tajiri duniani G7 utaofanyika nchini Canada.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.