Pata taarifa kuu
UFARANSA-ITLAIA-WAHAMIAJI

Ufaransa yaishtumu Italia kukataa kuwapokea wahamiaji

Wahamiaji 629, ikiwa ni pamoja na watoto wengi na wanawake, wamepata msaada kutoka kwa meli ya Aquarius, meli ya shirika la kihisani la SOS Méditerranée, katika pwani ya Mediterania, Juni 10, 2018.
Wahamiaji 629, ikiwa ni pamoja na watoto wengi na wanawake, wamepata msaada kutoka kwa meli ya Aquarius, meli ya shirika la kihisani la SOS Méditerranée, katika pwani ya Mediterania, Juni 10, 2018. Reuters
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameishutumu Serikali ya Italia kwa kutowajibika baada ya nchi hiyo kukataa kuwapokea wahamiaji na kuwaacha kwenye sintofahamu katika meli iliyokuwa imewaokoa kwenye bahari ya Mediterania.

Matangazo ya kibiashara

Meli ya Aquarius ambayo imebeba wahamiaji 629 itasindikizwa na meli nyingine mbili za jeshi la wanamaji wa Italia kuwapelekea wahamiaji hao nchini Uhispania kwenye mji wa Valencia ambako Serikali imekubali kuwapokea.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian ametupilia mbali madai kuwa nchi yake imekuwa ikikwepa kuwapokea wahamiaji na kuiachia Italia peke yake.

Haya yanajiri wakati huu maelfu ya wahamiaji wakiendelea kufanya safari za hatari kupitia bahari ya mediterania kuingia barani Ulaya kutafuta maisha na nchi ya Italia imekuwa kituo chao kikuu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.