ITALIA-UFARANSA-USHIRIKIANO

Di Maio: Italia yaendelea kusubiri Ufaransa kuomba msamaha

Mvutano waendelea kati ya Ufaransa na Italia, baada ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuhtumu kitendo cha Italia na kusema hakikubaliki.
Mvutano waendelea kati ya Ufaransa na Italia, baada ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuhtumu kitendo cha Italia na kusema hakikubaliki. REUTERS/Tony Gentile

Italia inaendelea kusubiri ufaransa kuomba msamaha baada ya ukosolewaji wa Paris kuhusu sera ya uhamiaji ya serikali ya Italia, makamu wa rais wa Baraza la serikali la Italia Luigi Di Maio, amesema.

Matangazo ya kibiashara

Mvutano kati ya Paris na Rome unaweza kusababisha kufutwa kwa mkutano uliopangwa Ijumaa wiki hii katika ikulu ya Elysee kati ya Emmanuel Macron na rais wa baraza la serikali Giuseppe Conte.

"Tunasubiri msamaha kutoka Ufaransa, na kama tukipata jambo hilo tutaweza kuanza ukurasa mpya," Luigi Di Maio amesem akwa vyombo vya habari. "Bado kuna wakati wa kupitia upya msimamo wetu, kuomba msamaha na kuanza upya."

Nathalie Loiseau, Waziri wa Mambo ya Ulaya wa Ufaransa, amesema Alhamisi hii asubuhi kwenye kituo cha Europe 1 kwamba rais wa Ufaransa na rais wa Baraza la serikali la Italia walizungumza "vizuri" Jumatano usiku.

Ziara ya Giuseppe Conte katika ikulu ya Elysee "haijathibitishwa wala haijasitishwa, tunataka aje," waziri wa mambo ya Ulaya wa Ufaransa ameongeza.

Italia na Malta zilikataa kuwakubali wakimbizi zaidi ya 600 waliokuwa wameokolewa Pwani ya Libya, lakini Uhispania iliamua kuwakubali.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alishtumu kitendo cha Italia na kusema hakikubaliki, matamshi ambayo yaliisababisha Italia kumwagiza balozi wa Ufaransa nchini humo.