Pata taarifa kuu
EU-WAKIMBIZI-USALAMA

Umoja wa Ulaya waafikiana kuhusu masuala ya wahamiaji

"Hatua zote zilizochukuliwa kuhusiana na vituo vitakavyodhibitiwa, ikiwa ni pamoja na kuhamishwa na kupelekwa sehemu nyingine vitafanyika kwa hiari," imesema taarifa iliyosainiwa na viongozi wa Ulaya baada ya saa tano za majadiliano.
"Hatua zote zilizochukuliwa kuhusiana na vituo vitakavyodhibitiwa, ikiwa ni pamoja na kuhamishwa na kupelekwa sehemu nyingine vitafanyika kwa hiari," imesema taarifa iliyosainiwa na viongozi wa Ulaya baada ya saa tano za majadiliano. REUTERS/Stéphanie Lecocq
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Baada ya saa kadhaa za majadiliano, hatimaye viongozi wa Umoja wa Ulaya waliokutana huko Brussels wameafikiana kuhusu masuala ya wahamiaji na hivyo kuepukana na mgogoro mpya.

Matangazo ya kibiashara

Italia imekua imezuia tangu Alhamisi jioni wiki hii kupitishwa kwa maazimio ya pamoja katika mkutano wa Umoja wa Ulaya wa Brussels, kwa kuomba nchi nyingine kujibu kwanza madai yake kuhusu suala la wahamiaji, hali ambayo ilitaka kuzua mgawanyiko mkubwa ndani ya Umoja wa Ulaya.

"Hatua zote zilizochukuliwa kuhusiana na vituo vitakavyodhibitiwa, ikiwa ni pamoja na kuhamishwa na kupelekwa sehemu nyingine vitafanyika kwa hiari," imesema taarifa iliyosainiwa na viongozi wa Ulaya baada ya saa tano za majadiliano.

Nchi hizo ishirini na nane za Umoja wa Ulaya pia zimeamua kuidhibiti mipaka yao ya nje, hasa kwa kuiongezea misaada Uturuki na Afrika Kaskazini, ili kuepuka kurudi kwa wimbi la wahamiaji na wakimbizi sawa na lile lililoshuhudiwa Ulaya mnamo mwaka 2015.

Taarifa hiyo inaonyesha pia kuwa mfumo wa kuanzishwa kwa "vituo vya mapokezi" vinavyopatikana nje ya eneo la Ulaya utafadhiliwa. Viongozi wa Ulaya pia wamekubaliana juu ya kuundwa kwa "vituo vitakavyodhibitiwa" ambapo yatajadiliwa maombi kuhusu hifadhi ya ukimbizi yatakayowasilishwa na wakimbizi.

Rais wa serikali ya Italia Giuseppe Conte, amekaribisha matokeo ya mkutano huo na kusema kuwa Italia haiko "peke yake". Roma itaamua baadaye ikiwa ni lazima au la kuwa na vituo vya mapokezi kwa wahamiaji, ameongeza.

Akizungumza baada ya mkutano huo, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alizungumzia "nia ya kulinda vema mipaka na kuimarisha sheria za mapokezi".

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.