UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO

Waziri mwenye dhamana ya Uingereza kujitoa EU ajiuzulu

Waziri wa Uingereza wa masuala ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, David Davis, huko Brussels (picha ya kumbukumbu).
Waziri wa Uingereza wa masuala ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, David Davis, huko Brussels (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Francois Lenoir

Waziri wa masuala ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya David Davis amejiuzulu. Katika barua yake ya kujiuzulu ameeleza kwamba hataki kuwa pingamizi katika mpango wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, mpango unaotakiwa na Waziri mkuu Theresa May.

Matangazo ya kibiashara

Katika barua yake hiyo, David Davis amesema msimamo wa Downing Street kuhusu Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya pia ni "dhaifu" kwa mtazamo wake.

Msimamo huo "dhaifu" unaokosolewa na David Davies, ni rasimu mpya iliyotolewa na Theresa Mey kwa serikali ya Uingereza siku mbili zilizopita na ambayo imepelekea kutangazwa kwa makubaliano kuhusu nia ya kudumisha uhusiano wa kibiashara na Umoja wa Ulaya baada ya Uingereza kujitoa katika umoja huo.

Makubaliano hayo yanaeleza mipango ya kuanzisha eneo la biashara huria na utaratibu kuhusu masuala ya ushuru na nchi ishirini na saba wanachama wa umoja huo, ili kuendelea na biashara hiyo bila kuepo na "mgawanyiko" na bara la Ulaya. Makubaliano ambayo hayawaridhishi "wanaharakati wanaotaka Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya" na mmoja wa wawakilishi wao wenye ushawishi mkubwa, David Davis.

Hajazungumza chochote katika barua yake ya kujiuzulu. "Maslahi ya taifa yanahitaji waziri wa masuala ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya aambaye anaamini mpango wako, si tu kuwa "pingamizi," Davis Davis ameandika katika barua yake ya kujiuzulu.