UFARANSA-USALAMA

Kesi ya Benalla: Ikulu ya Elysee yakabiliwa na shutma kali

Rais Emmanuel Macron, Waziri wa Mambo ya Ndani Gerard Collomb (kulia) na Alexandre Benalla (nyuma), Juni 20, 2017.
Rais Emmanuel Macron, Waziri wa Mambo ya Ndani Gerard Collomb (kulia) na Alexandre Benalla (nyuma), Juni 20, 2017. Benjamin CREMEL / AFP

Waziri wa Mambo ya Ndani Gérard Collomb na mkuu wa polisi wa Paris Michel Delpuech walijibu Jumatatu, Julai 23 maswali ya wabunge wa Tume ya Sheria ya Bunge ili ili kupata ukweli wa mambo kuhusu kesi ya Benalla.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya ndani nchini Ufaransa Gerard Collomb amewaambia wabunge ni kwanini hakumchukulia hatua mlinzi wa rais Emmanuel Macron baada ya kumpiga mwanadamanaji.

Gerard Collomb na Michel Delpuech wamejitetea wakisema kuwa mlinzi huyo wa rais Macron alishindwa kujizuia. Hata hivyo wamesem ahawawezi kuongelea mambo yasiyowahusu.

Collomb ambaye amekuwa akipata shinikizo za kujiuzulu kwa kutochukua hatua yoyote, amesema aliona mkanda ulionesha namna mlinzi huyo alivyoshambulia mwanadamanaji na kuiachia Ofisi ya rais Macron kumchukulia hatua.

Kwa upande mwingine, Waziri wa Mambo ya Ndani na mkuu wa polisi katika mji wa Paris walihojiwa na wabunge wa tume ya Sheria ambayo ilitaka kuelewa jinsi Alexandre Benalla, mshiriki wa karibu wa Emmanuel Macron, alijikuta akiwapiga waandamanaji kando ya CRS wakati wa maandamaano ya siku kuu ya wafanyikazi Mei mosi mwaka huu. Na hasa kwa nini hakuna mtu yoeyote aliyeweza kufungua mashitaka baada ya kupata taarifa hiyo. Kwa sababu Ibara ya 40 ya Kanuni ya Utaratibu wa sheria ya Uhalifu ikowazi: afisa yeyote ambaye atapata taarifa inayohusiana na uhalifu lazima atoe taarifa kwa mwendesha mashitaka wa Jamhuri.

Mlinzi huyo Alexandre Benalla, mwenye umri wa miaka 26, amefunguliwa mashtaka yakiwemo, kuingilia kazi ya Polisi.