UINGEREZA-AJALI-USALAMA

Mtuhumiwa wa shambulio la London atambuliwa

Polisi ya London hauikutoa maelezo zaidi kuhusu mtuhumiwa, lakini imesema kuwa ni raia wa Uingereza mwenye asili ya Sudan.
Polisi ya London hauikutoa maelezo zaidi kuhusu mtuhumiwa, lakini imesema kuwa ni raia wa Uingereza mwenye asili ya Sudan. REUTERS/Henry Nicholls

Mtu aliyekamatwa baada ya kuwagonga wapita njia siku ya Jumanne huko London, nchini Uingereza, ni raia wa Uingereza mwenye asili ya Sudan, polisi ya Uingereza imesema leo Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa chanzo cha idara ya usalama ya Ulaya, mtu huyo anaitwa Salih Khater na alikua hajulikani kwenye idara ya usalama ya Uingereza kabla ya shambulizi dhidi ya wapita njia mbele ya Bunge la Westminster.

Watu watatu walijeruhiwa katika tukio hilo lakini wanaendelea vizuri.

Polisi ya London hauikutoa maelezo zaidi kuhusu mtuhumiwa, lakini imesema Jumatano wiki hii ni raia wa Uingereza mwenye asili ya Sudan.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 29, alikamatwa katika eneo la tukio chini ya Sheria ya Ugaidi ya mwaka 2000 na kuzuiliwa kwa madai ya kula njama, maandalizi na kujihusisha na vitendo vinavyoshukiwa kuwa vya kigaidi. Polisi ya Uingereza imesema leo Jumatano kuwa anashtumiwa pia kujaribu kuua.

"Kipaumbele cha wachunguzi ni kuelewa hasa sababu za tukio hili," polisi imeongeza.

Mtuhumiwa amekataa kushirikiana na wachunguzi. "Kutokana na ukweli kwamba kitendochake kinaonekana kuwa amekitekeleza kwa makusudi. Kesi hiyo inachukuliwa kama tukio la kigaidi na uchunguzi unaongozwa na maafisa wa kikosi cha kupambana na ugaidi, "imesema taarifa hiyo.

Msako ulifanyika siku ya Jumanne katika sehemu tatu tofauti, operesheni mbili katika mji wa Birmingham na moja huko Nottingham. Moja ya opereheni hiyo inmeendelea leo Jumatano huko Birmingham, operesheni nyingne mbili zimemalizika.

Polisi ya Uingereza wanasema watu wawili waliojeruhiwa na kulazwa hospitali wameruhusiwa kwenda nyumbani. Mtu wa tatu aliyejeruhiwa alitibiwa jana Jumanne katika eneo la tukio.