ITALIA-AJALI-MAZINGIRA

Waokoaji waendelea kutafuta watu waliokwama Genoa Italia

Helikopta ya kikosi cha Zima Moto cha Italia ikipita mbele ya daraja lililovunjika huko Genoa, Agosti 14, 2018.
Helikopta ya kikosi cha Zima Moto cha Italia ikipita mbele ya daraja lililovunjika huko Genoa, Agosti 14, 2018. REUTERS/Massimo Pinca

Shughuli ya uokoaji inaendelea huko Genoa, kaskazini mwa Italia, baada ya kuvunjika kwa daraja la barabara ya mwendo kasi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30. Waziri wa usafirishaji Danilo Toninelli ameliongelea janga hilo kuwa kubwa.

Matangazo ya kibiashara

Magari zaidi ya 30 yalianguka katika upande wa mfereji wa uchafu.

Wafanyakazi wa dharura wanajaribu kuwatafuta watu walioanguka na magari yao huku wakiwa wanasaidiana na mbwa wenye utaalamu kwa kunusa.

Sauti za kuomba msaada kutoka kwa watu wanaosadikiwa kunaswa katika mabaki ya daraja hilo zimesikika usiku kucha.

Ufaransa imehaidi kushirikiana pamoja na Italia katika janga hilo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameandika ujumbe wa pole katika ukurasa wake wa Twitter kwa raia wa Italia na Ufaransa.

Daraja hilo ambalo lilijengwa tangu mwaka 1960,l ilikuwa linawahudumia raia wa Italia na Ufaransa.

Naibu waziri wa usafirishaji wa nchi hiyo ,Edoardo Rixi amesema idadi ya vifo ni 35 lakini wanatarajia kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka.