ITALIA-AJALI-MAZINGIRA

Italia yatangaza hali ya dharura kwa mwaka mmoja Genoa

Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte (katikati), akiongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani Matteo Salvini (D) na Waziri wa Kazi na Viwanda Luigi Di Maio, ametangaza mfululizo wa hatua zilizochukuliwa na serikali yake baada ya vifo vingi kutokea huko Genoa.
Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte (katikati), akiongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani Matteo Salvini (D) na Waziri wa Kazi na Viwanda Luigi Di Maio, ametangaza mfululizo wa hatua zilizochukuliwa na serikali yake baada ya vifo vingi kutokea huko Genoa. REUTERS/Stefano Rellandini

Serikali ya Italia imetangaza hatua kadhaa baada ya kuvunjika kwa daraja huko Genoa, nchini Italia na kusababisha vifo vingi. Hali ya dharura imetangazwa katika eneo hilo na itadumu mwaka mmoja kwa mujibu wa serikali ya Jimbo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashahidi hakuna matumani ya kuwapata tena watu walio hai.

Watu wasiopungua 39 walipoteza miasha katika tukio hilo. Uchunguzi wa kupata wahusika umeanza. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Italia, mtaalamu mmoja alikuwa ameonya muda mrefu kuhusu jinsi gani daraja hilo lilijengwa kimakosa kabla ya tukio hilo.

Kwa ombi la serikali ya Jimbo la Genoa, "tumetangaza hali ya hatari kwa miezi 12," amesema Waziri Mkuu wa Italia, Giuseppe Conte, baada ya kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri huko Genoa.

Hali hii ya dharura inatoa "mfumo wa kawaida" kwa usimamizi wa eneo la tukio na usaidizi kwa watu zaidi ya 630 waliookolewa ikiwa ni pamoja na nyumba amesema rais wa jimbo la Genoa, Giovanni Toti.

Daraja lilivunjika hiko Genoa.
Daraja lilivunjika hiko Genoa. REUTERS/Stefano Rellandini

Serikali itatoa msaada kwa waathirika. Hii pia inairuhusu kutoa misaada ya dharura ya euro milioni 5. Waziri Mkuu pia ametangaza siku moja ya maombolezo ya kitaifa itakayoendana sambamba na sherehe ya mazishi. lakini tarehe haijatangazwa.