MALI-UFARANSA-SIASA-MAZINGIRA

Waziri wa Mazingira wa Ufaransa ajiuzulu

Waziri wa Ufaransa mwenye dhamana ya Ikolojia na Mshikamano, Nicolas Hulot, ametangaza nia yake ya kujiuzulu kwenye nafasi yake, mwaka mmoja baada ya uteuzi wake.

Waziri wa Mazingira wa Ufaransa Nicolas Hulot.
Waziri wa Mazingira wa Ufaransa Nicolas Hulot. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Nicolas Hulot amesema kwenye radio France Inter kuwa amekua akijihisi "peke yake katika shughuli" zinazohusiana na masuala ya mazingira.

"Nimechukua uamuzi wa kujiuzulu," Nicolas Hulot ametangaza kwenye radio France Inter Jumanne hii Agosti 28, 2018.

Mtayarishaji huyo wa zamani wa makala kwenye televisheni amesema kuwa amechukua hatua hiyo bila hata hivyo kumshauri rais Macron na Waziri Mkuu Philippe kwa kuhofia kuwa wanaweza kumuzuia kuchukua hatua hiyo.

"Ni uamuzi mzuri wa uaminifu," amesema waziri Hulot.

"Waziri Mkuu, Rais wa Jamhuri, waliniamini kwa miezi yote hiyo 14," amesema Nicolas Hulot kwenye radio France Inter. Lakini kwa mtazamo wake, serikali haijaweza kuzingatia masuala ya mazingira.