UHISPANIA-WAHAMIAJI-USALAMA

Wahamiaji 700 waokolewa kwenye Pwani ya Uhispania

Meli ya Aquarius iliyobeba wahamiaji zaidi ya 600 ikiwasili kwenye bandari ya Valencia, Juni 17, 2018.
Meli ya Aquarius iliyobeba wahamiaji zaidi ya 600 ikiwasili kwenye bandari ya Valencia, Juni 17, 2018. © AFP

Waokoaji katika bahari ya uhispania wamefanikiwa kuwokoa wahamiaji 675 mwishoni mwa juma hili lililopita kati ya Morocco na Uhispania, nchi ambayo wahamiaji haramu wengi wanaingilia kuelekea Ulaya, msemaji wa serikali ameliambia shirika la Habari la AFP.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya wahamiaji 405 waliokolewa siku ya Jumamosi, wahamiaji 270 waliokolewa jana Jumapili, wakiwa katika boti saba, chanzo hicho kimeomgeza.

"Watoto au watoto wachanga saba" walikua miongoni mwa abiria, ambao nusu yao ni kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara na nusu wengine kutoka nchi za Maghreb, kwa mujibu wa chanzo hicho.

Waokoaji hawakuwa na taarifa yoyote kuhusu wahamiaji hao waliokuwa wametoweka au waliokuwa katika hali mba ya afya.

Uhispania mwaka huu, imekuwa nchi ya kwanza ambapo wahamiaji wengi wanapitia kuelekea Ulaya, baada ya Italia kufunga mipaka yake chini ya shinikizo la waziri wake wa Mambo ya Ndani, Matteo Salvini.

Wahamiaji zaidi ya 40,000 wameingia Uhispania tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ikiwa ni pamoja na 35,000 waliosafiri kupitia baharini na karibu 5,000 waliopitia nchi kavu, wakiingilia katika mji wa Uhispania wa Ceuta na Melilla nchini Morocco, kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).

Wahamiaji zaidi ya 1,700 wamepoteza maisha au wkutoweka katika bahari ya Mediterranean tangu mwanzoni mwa mwaka hu, ikiwa ni pamoja na 362 katika pwani ya Uhispania, kwa mujibu IOM.