UFARANSA-MAANDAMANo-UCHUMI

Wafanyakazi waliostaafu waandamana dhidi ya Emmanuel Macron

Maandamano dhidi ya mageuzi ya serikali, Oktoba 9, 2018, Paris, Ufaransa.
Maandamano dhidi ya mageuzi ya serikali, Oktoba 9, 2018, Paris, Ufaransa. REUTERS/Gonzalo Fuentes

Vyama kadhaa vya wafanyakazi vimetoa wito wa kuandamana Jumanne hii Oktoba 9, 2018 dhidi ya sera ya kijamii ya Rais Emmanuel Macron. Sekta zote zimetolewa wito wa kushiriki maandamano hayo ya amani.

Matangazo ya kibiashara

Vyama kadhaa vya wafanyakazi vimetoa wito wa kuandamana Jumanne hii Iktoba 9, 2018 dhidi ya sera ya kijamii ya Rais Emmanuel Macron. Sekta zote zimetolewa wito wa kushiriki maandamano hayo ya amani.

Wafanyakazi waliostaafu, ambao wanahisi kuwa wameumizwa na marekebisho yanayoendelea wametakiwa kushiriki kwa wingi katika maandamano hayo.

Wafanyakazi waliostaafu wanataka kutetea uwezo wao katika mambo ya ununuzi dhidi ya maamuzi mawili ya Emmanuel Macron.

Uamuzi wa kwanza unahusu ongezeko la CSG, mchango wa kijamii kwa watu wote. Kodi ambayo Rais Macron amongeza kwenye pensheni za kustaafu kwa asilimia 1.7 tangu mwezi Januari mwaka huu ili kuziba pengu kwa mchango wa ukosefu wa ajira na michango ya ugonjwa kwa wafanyakazi binafsi.

Ongezeko hili linahusu 60% ya wafanyakazi waliostaafu. Jambo al pili linahususuala la kusitisha au kuzuiwa pensheni: pensheni huongezeka kwa kiasi cha gharama za maisha. Lakini hapana mwaka 2019 au 2020: kwa miaka miwili ijayo, watu waliostaafu wataongezeka kwa 0.3%, ikilinganishwa na mfumuko wa bei wa 1.6% kulingana na utabiri.