UFARANSA-UJERUMANI-EU-USALAMA

Macron na Merkel waonyesha msimamo wao wa pamoja kuhusu jeshi la Ulaya

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wasema Ulaya inahitaji kuwa na jeshi la pamoja kwa kukabiliana na adui.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wasema Ulaya inahitaji kuwa na jeshi la pamoja kwa kukabiliana na adui. Tobias SCHWARZ / AFP

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wanakutana jijini Berlin, kuonesha mshikamano na umoja wa nchi zao dhidi ya kile kinachoonekana kama kuongeza kwa umaarufu wa rais wa Marekani Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

Huu ni mkutano wa pili kwa kipindi cha wiki moja, kati ya viongozi hawa wawili wenye mataifa yenye nguvu barani Ulaya.

Merkel na Macron walikutana jijini Paris siku chache zilizopita, na kusema kuwa nchi zao zitaendelea kushirikiana kuhakikisha kuwa bara la Ulaya linasimama na kujitegemea katika masuala mbalimbali lakini pia kuwa na ushawishi duniani.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema bara la Ulaya ni lazima liwe imara na kujitegemea ili kutekeleza jukumu lake la kuzuia machafuko katika masuala ya dunia.

Macron ametoa kauli hii jijini Berlin wakati, akiwahotubia wabunge wa Ujerumani na kuwaambia kuwa, ushirikiano wa nchi yake na Ujerumani, ni lazima usaidia dunia iisingie kwenye mgogoro, na hivyo ni lazima bara la Ulaya liwe dhabiti.

Wito huu umekuja, baada ya siku chache zilizopita, rais huyu kusema kuwa bara la Ulaya linastahili kuwa na jeshi imara dhidi ya Marekani, Urusi na China, kauli ambayo ilimkera rais Donald Trump. ambaye kupitia ukurasa wake wa Twitter, alisema matamshi ya Macron hayakubaliki.