UE-BREXIT

Wapinzani wa Brexit kuhudhuria mkutano wa Democratic Unionist hii leo

Waziri wa zamani wa mambo ya kigeni wa Uingereza, Boris Johnson, akizungumza kwenye bunge la Congress huko Birmingham mnamo Oktoba 2, 2018.
Waziri wa zamani wa mambo ya kigeni wa Uingereza, Boris Johnson, akizungumza kwenye bunge la Congress huko Birmingham mnamo Oktoba 2, 2018. REUTERS/Darren Staples

Wapinzani wa rasimu ya makubaliano ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya inayotarajiwa kupitishwa na viongozi wa Umoja wa Ulaya watatawala mkutano wa leo Jumamosi wa Chama cha Democratic Unionist, chama cha Kaskazini cha Ireland ambacho msaada wake ni muhimu kwa mipango ya Serikali ya Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May nampango wa kujiondoa Umoja wa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Uingereza, Boris Johnson, mkosoaji mkuu wa mpango huo, atahudhuria - pamoja na Fabian Picardo, Waziri Mkuu wa Gibraltar, ambayo pia inaweza kudhoofisha mkutano wa Jumapili wa Umoja wa Ulaya.

Viongozi wa Mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya, watakutana siku ya Jumapili jijini Brussels nchini Ubelgiji, kujadili na kupitisha makubaliano yaliyoafikiwa kati ya Uingereza na wakuu wa Baraza hilo kuhusu namna watakavyojitoa katika Umoja huo mwezi Machi mwaka 2019.

Makubaliano hayo yamewakasirisha wabunge nchini Uingereza ambao wengi wamesema hawakubaliani nayo na wanamtaka Waziri Mkuu Theresa May, kufanya mazungumzo mapya.

Hata hivyo, May kwa mara nyingine amesema kuwa, makubaliano hayo ni mazuri kwa ajili ya maendeleo ya Ungereza na ushirikiano wake wa siku zijazo na mataifa mengine ya bara Ulaya.