EU-UINGEREZA-ULAYA-SIASA

Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya wanakutana kupitisha mkataba wa Uingereza kujiondoa

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker, akizungumza hivi karibuni katika mkutano wa viongozi wa Umoja huo
Mkuu wa Tume ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker, akizungumza hivi karibuni katika mkutano wa viongozi wa Umoja huo REUTERS/Vincent Kessler

Viongozi wa mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya, wanakutana jijini Brussels nchini Ubelgiji, kujadili na kupitisha mkataba wa makubaliano kati ya Uingereza na wakuu wa EU, kuhusu ushirikiano utakavyokuwa baada ya Uingereza kuondoka rasmi mwezi Machi mwaka 2019.

Matangazo ya kibiashara

Matumaini ya viongozi hao kukubaliana yamekuja baada ya mwafaka kupatikana kuhusu kisiwa cha Gibraltar, amacho kwa muda mrefu kimekuwa kikizozaniwa kati ya Uingereza na Uhispania.

Hatua hii inakuja, baada ya majadiliano magumu ya miezi 17 kati ya serikali ya Uingereza na wakuu wa EU kuhusu hali itakavyokuwa kuhusu biashara, ajira, usalama miongoni mwa mambo mengine, baada ya kuondoka kwa Uingereza.

Hata hivyo, kuna wasiwasi kuwa, wabunge wa Uingereza wataukataa mkataba huo hata ukipitishwa na wakuu wa nchi za Umoja wa Ulaya, baada ya wiki iliyopita kuonesha masikitiko yao.

Viongozi kadhaa wa Umoja wa Ulaya wakiongozwa na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, amesema, mkataba huo ni mzuri kwa mustakabali wa EU na Uingereza, kauli ambayo imeungwa mkono na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May.