Waandamanaji na polisi wakabiliana jijini Paris, kupinga nyongeza ya bei ya mafuta
Imechapishwa:
Rais wa Ufaransa Emmmanuel Macron, amewashtumu waandamanaji waliokabiliana na maafisa wa polisi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo siku ya Jumamosi, wakati wakiandamana kupinga kupanda kwa bei ya mafuta.
Macron, amesema ilikuwa ni aibu kubwa kwa waandamanaji kuanza kukabiliana na maafisa wa polisi.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, rais Macron amesema, "Hakuna nafasi kwa machafuko katika Jamhuri ya Ufaransa,".
“Hatuko hapa, kupigana na polis. Tulikuja kwa sababu tunataka serkali itusikie,” alisema Laetitia Dewalle mmoja wa wasemaji wa waandamanaji.
Maandamano haya yameingia wiki ya pili, huku waandamanaji wakivalia vazi maalum la njano, linalotumiwa na wafanyikazi wanaofanya kazi katika sekta ya mafuta.
Polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji, waliokuwa wanachoma matairi katika barabara maarufu ya Champs-Elysées.
Waandamanaji zaidi ya 100, 000 walijitokeza kushiriki katika maandamano hayo.