EU-UINGEREZA-ULAYA-SIASA

Waziri Mkuu Theresa May kukutana tena na Mawaziri baada ya viongozi wa EU kuridhia mkataba

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May akiwa katika makao makuu ya Umoja wa Ulaya jijini Brussels nchini Ubelgiji
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May akiwa katika makao makuu ya Umoja wa Ulaya jijini Brussels nchini Ubelgiji REUTERS/Piroschka van de Wouw

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May siku ya Jumatatu anakutana na Baraza la Mawaziri, baada ya mkataba wa nchi hiyo kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, kukubaliwa na kuidhinishwa na viongozi 27 wa Umoja huo.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao walikutana jijini Brussels nchini Ubelgiji na kuidhinishwa makubaliano hayo, baada ya miezi 17 ya mazungumzo magumu ya namna Uingereza itakavyoshirikiana na mataifa mengine ya Ulaya, baada ya kujiondoa mwezi Machi mwaka 2019.

May na viongozi wa EU wamesema, kuwa mkataba huo utakuwa wa manufaa makubwa kwa nchi yake na Umoja wa Ulaya kuhusu masuala ya biashara, usalama na ajira miongoni mwa mambo mengine.

Hata hivyo Bi. May, bado anakabiliwa na vita kali ya kupata ridhaa ya wabunge kabla ya kupiga kura juma lijalo.

Wabunge wiki iliyopita, waliukataa makataba huo baada ya Waziri Mkuu kuuwasilisha bungeni, wengi wakisema kuwa, hauheshimu uamuzi wa wananchi wa taifa hilo ambao mwaka 2016, waliamua wanaondoka katika Umoja huo.