UFARANSA-MAANDAMANO-SIASA-KODI

Hofu ya maandamano yatanda nchini Ufaransa

Waandamanaji jijini Paris nchini Ufaransa
Waandamanaji jijini Paris nchini Ufaransa Fuente: AFP.

Usalama umeisharishwa nchini Ufaransa, hasa jijini Paris kwa hofu ya kushuhudiwa tena kwa maandamano, ya kupinga nyongeza ya kodi kwa bidhaa ya  mafuta.

Matangazo ya kibiashara

Rais Emmanuel Macron ametoa wito kwa waandamanaji kutojitokeza, kwa kile alichosema kuwa serikali imesikia kilio chao na inashughulikia madai yao.

Hata hivyo, wanaoandaa maandamano haya, wanasema yataendelea kwa sababu wanataka serikali kuchukua hatua zaidi.

Jumamosi kadhaa, zilizopita, maandamano haya yaliyoanza mwezi Novemba yamegeuka kuwa makabiliano makali kati ya waandamanaji na polisi, huku uharibu mkubwa ukiripotiwa hasa katika jiji la Paris.

Mechi kadhaa za ligi kuu nchini humo zimeahirishwa kwa hofu ya machafuko.