UFARANSA-MAFUTA-MAANDAMANO-MACRON

Waandamanaji nchini Ufaransa wakataa kumti rais Macron

Maandamano jijini Paris nchini Ufaransa 8/12/2018
Maandamano jijini Paris nchini Ufaransa 8/12/2018 REUTERS

Waandamanaji walijitokeza siku ya Jumamosi  jijini Paris na miji mingine nchini Ufaransa kuendelea kupinga nyongeza ya kodi kwa mafuta, licha ya wito wa rais Emmanuel Macron kuwa wasijitokeze.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, idadi ya waandamanaji ilkuwa ndogo ikilinganishwa na Jumamosi zilizopita.

Waandaaji wanasema ni waandamanaji eldu 66 ndio waliojitokeza ikilinganishwa na 125,000 waliokuwepo Jumamosi iliyopita.

Mbali na suala la nyongeza ya kodi ya mafuta, waandamanaji hao sasa wanataka mabadiliko katika sekta ya elimu miongoni mwa mambo mengine.

Watu saba wamepoteza maisha katika maandamano hayo ya kila Jumamosi, huku mamia wakikamatwa.

Rais Emmanuel Macron amesema anawaelewa waandamanaji na kuwaomba waachane na maandamano hayo ya kila Jumamosi.