UFARANSA-SIASA

G7: Le Drian aeleza malengo ya uongozi ujao wa Ufaransa Biarritz

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian Desemba 14, 2018.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian Desemba 14, 2018. REUTERS/Danish Siddiqui

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amewasilisha falsafa ya uongozi ujao wa Ufaransa katika Jumuiya ya nchi tajiri duniani G7 utakanyika mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka 2019 katika mji wa Biarritz kusini-magharibi mwa Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambae ndie alitarajiwa kwenda huko Biarritz lakini alifuta safari yake baada ya kufanya mashauriano na washikadau mbalimbali kushughulikia swala la waandamanaji .

Waziri Le Drian amesema kupungua kwa hali ya kutokuwa na usawa ni sehemu ya malengo ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa, lakini inahitaji kujitoa zaidi.

Hata hivyo baadhi ya watu wamekosoa hatuwa ya rais Emmanuel Macron ya kufuta safari yake huko Biarritz wakiona kwamba kulikuwa na uwezekano wa mawaziri wake kuendelea kufanya mashauriano na wadau mbalimbali.